PATANISHO: Mume wangu huniita scare crow

Claire alituma ujumbe akisema angependa kupatanishwa na mumewe bwana Joseph.

"Huyu mzee wangu tunakosana kila wakati kwani huwa ananishuku kuwa nina mpango wa kando lakini ni ukweli ninaye." Alisema Claire huku akidai kuwa anataka tu kumuomba mumewe msamaha.

Nataka tu kumuomba msamaha kwani yeye huja kwa boma na ananiita scare crow huku akinitusi matusi kali kali mengine siwezi sema hewani."Aliongeza huku akidai mumewe humchukulia kama mtoto kwa nyumba.

"Huyo mpango wangu wa kando ni wa kuzungumza tu naye lakini hakuna chochote ambacho nimewahi fanya naye." Alisema.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wamejaliwa watoto wawili pamoja.

Juhudi zetu za kumtafuta bwana Joseph hazikufua dafu.