PATANISHO: Mume wangu hushughulikia mke wa pili pekee

Joyce, 38, alituma ujumbe akisema kuwa angependa apatanishwe na mumewe bwana Caleb, 46, ambaye walikosana mwaka wa 2011.

"Tulikosana karibu miaka kumi lakini nilirudi kwake 2018, vile nilirudi ameniacha tu hapo na ingawa anashughulikia watoto mimi hanishughulikii na huwa haonekani nyumbani." Alijitetea Joyce.

Alidai kuwa wamejaribu kusuluhisha hata kwa njia ya kuita wazazi lakini hamna lililobadilika na isitoshe ana mke mwingine.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka ishirini.

Tulipomtafuta bwana Caleb, alijibu simu ila hakutaka kuzungumza na mkewe kwani alikatiza mawasiliano kati yetu.

Joyce alidai kuwa walipotengena, Caleb alileta mke mwingine nyumbani baada ya wiki mbili na hapo ndipo mambo yalibadilika, sasa hivi yeye hununua vitu nyumbani ila huwa hamshughulikii.

"Nampenda na namheshimu kama mke wangu na ningependa arudi tulee watoto wetu pamoja." Huo ndio ulikuwa ujumbe wa Joyce wa mwisho baada ya juhudi zetu kumtafuta Caleb kugonga mwamba.