patanisho.fresh

PATANISHO: Mume wangu hutaka tufanye mapenzi hadi nikiwa na periods

Faith alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Sam ambaye walikosana sana Jumatatu iliyopita.

Mzee wangu tumekuwa tukisumbuana kuhusu mapenzi kwa nyumba kwani hutaka tufanye mapenzi kila siku, hata nikiwa na period zangu yeye hajali. Alieleza.

Patanisho: Mpango wa kando wa bibi yangu anampigia simu tukiwa tumelala

Nikamwambia haya maisha yamekuwa ngumu kwani nalima kwa shamba na nalea watoto na sitaweza. Isitoshe nilimuomba aoe mke wa pili anisaidie kwani siwezi.

Siku moja niliamka kwenda kumshughulikia mtoto na alinizaba kofi akisema namwonesha madharau. Hapo nikatoroka na niakenda nyumbani. Aliongeza Faith huku akiwa na wingi wa huzuni.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane na wamefanikiwa na watoto.

PATANISHO: Ndugu yangu alihepa majukumu ya kuwasaidia wazazi

Bwana Sam alipopigiwa simu alisema kuwa mkewe alimtishia kuwa atamuua na atampa madawa fulani.

Faith alisema kuwa anampenda mumewe na kuwa aliwacha shule ili aolewe na bwana Sam licha ya wazazi wake kupinga ndoa hiyo.

Siko tayari kurudiana naye kwani nina machungu, aniwache nitulie na nifikirie ili nijue kama tutarudiana, kwa sasa mapenzi yako kwa watoto.

PATANISHO: Mume wangu akilewa hutishia kuniua na nikaamua nikimbie

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments