PATANISHO: Mume wangu kila mara hutishia kunikata kata

Siku ya Jumanne, Geoffrey alituma ujumbe akiomba ndoa yake ya miaka 13 iokolewe akidai kuwa mkewe aliondoka na kumuachia watoto wiki nne zilizopita akienda kumuona babake na hajarudi bado.

Geoffrey alieleza,

Baba alikuwa mgonjwa na anikamwambia kwa sababu siku zimesalia mbili kabla ya shule kufungwa asubiri lakini alipoenda kazini aliniarifu yuko safarini akielekea nyumbani.

Alienda kumuona baba hospitalini na pia mimi nilienda kumuona, hata hivyo wazazi wake walisema kuwa kuna kitu nilimfanyia na hawawezi mruhusu arudi kwangu.

Aliongeza,

Kuna nyumba fulani naishi na nikama ina mashetani kwani watu hukuwa wagonjwa, bibi akipata mtoto ana shida kadhaa, watu wanasota. Mimi nilikuwa mtu wa kanisa na kuna siku nilianza kutembea kama mtu amelewa na hospitalini niliambiwa kuwa sina damu mwilini.

Geoffrey anadai kuwa alianza kupoteza fahamu na aka katakata tuktuk ya shilingi 400,000 na kuiuza kwa shilingi elfu saba.

Mkewe Geoffrey anaitwa mama Eliza.

Katika miaka hiyo yote hajawahi nipa uhuru wa kwenda nyumbani na isitoshe mimi ndio hujishughulisha na naishi kama sina mwanaume." Alisema Mama Eliza.

Aliongeza, "Nilimwambia nina fare na nataka kwenda nyumbani kumuona babangu sahii napangia kufua kisha niende Kitale kulima.

Sitarudi kwake lakini uzuri wiki iliyoisha aliniletea kitinda mimba wetu lakini kuna siku yeye hunitishia kuwa atanikata kata kama yule msichana wa University mara atanikata mikono. Aliongeza mkewe Geoffrey.