PATANISHO: Mume wangu ndiye alifanya nianze kunywa chang'aa

IMG_9062
IMG_9062
Jackie mwenye umri wa miaka 27, aliomba apatanishwe na mumewe bwana Dickson, 36.

Sisi tumekaa naye kwa miaka miwili vizuri na kuna wakati alikuwa anaongea na wanawake kama siko na wakati mwingine anapigwa picha na wanawake na kuzileta kwa nyumba.

Aliongeza,

Hapo tukakosana na yeye aliondoka na kuniacha kwangu, ningependa kumuomba msamaha kwani pia mimi nilimkosea kwa kuanza ulevi. Hata hivyo, yeye ndiye aliyefanya nianze kulewa kwani nilikuwa na stress juu hata akija nyumbani hakuwa anaona kama mimi ni mtu.

Wawili hao bado hawajafanikiwa na mtoto lakini Jackie aliingia kwa ile ndoa na mtoto.

"Mimi nilishakusamehe, si nilikwambia nimekusamehe? Hiyo maneno nilisahau tafadhali." Dickson alimwambia Jackie akisema kuwa amekata kauli tayari kuwa wawili hao hawatorudiana.

Dickson aliongeza,

Ilifika mahali alitaka kupigana nami na nilimuacha aendelee na maisha yake.

Isitoshe Jackie alitishia kujitoa uhai kwake akisema haelewi mbona Dickson hamsamehei licha yake kumsamehe mara kadhaa hapo awali. Anakiri kuwa mumewe anapewa ushauri mbaya na anaamini bado anampenda.

&feature=youtu.be