PATANISHO: Mume Wangu Ni Mhanyaji Kupindukia

Bwana Munene alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Wanjiru akidai wawili hao walikosana "Kwa ajili ya kufuata maneno ya watu."

"Mke wangu tulikosana naye mwezi wa saba kwa sababu huwa haniamini hata nikimuambia ukweli husema nadanganya. Wakati hatukuwa tumepatana nilikuwa na rafiki mwanadada kwani nilikuwa nimekomboa nyumba kwao mjini Nakuru.

Sasa nilipofika Nakuru nikapatana na Wanjiru na tukafunga ndoa bila kumjulisha yule mwanadada wa Molo.

Siku moja yule mwadada akapiga simu na mke wangu alipojibu yule mwanadada wa Nakuru alijitambulisha kama bibi ya Bonnie, na kila ninapomweleza mke wangu ukweli bado haniamini." Alijieleza bwana Munene.

Alipopigiwa simu bi Wanjiru aliwashtua wengi alipodai kuwa sahii hana bwana na kuwa ameamua kuishi pekee yake.

"Unajua siku hizi mtu anafaa kuishi pekee yake juu hakuna stress na madharau ndogo ndogo." Alisimulia Wanjiru.

Alikuwa na uhusiano na huyo msichana na kulingana navile alikuwa anaongea ilifika wakati sisi sote tukapangwa na mori na akasema kuwa yule alikuwa mpenzi wake, isitoshe alikuwa anasafiri hadi Nakuru." Aliongeza huku akidai kuwa bwanake ana tabia ya kupenda wanawake.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be