PATANISHO: Mume wangu ni mtu wa fujo kila anapolewa

Bwana Fred ndiye aliyeomba kupatanishwa siku ya Jumanne akidai yeye na mkewe bi Nancy, walikosana mwezi Julai na amebaki mpweke kusononeka akidai kuwa anakaribia kujitia kitanzi.

"Nilikuwa nimerudi nyumbani nikiwa mlevi na tukabishana hadi nikampiga, kesho yake kurudi nyumbani nilipata amepakia kila kitu na kwenda kwao. Awali alikuwa amebeba mtoto." Alieleza Fred ambaye ameishi kwa ndoa kwa miaka sita.

Kulingana na Fred sio mara ya kwanza kumpiga na sasa anahisi ni kama hana thamani.

Nilipata message kwa simu yake mtu akimtongoza na licha ya kuto reply nilishikwa na wivu sana. Sikuona aki reply lakini nilihisi nikama alikuwa ananidanganya." Aliongeza.

Anasema kuna wakati walikuwa wanazungumza lakini mkewe akamblock na isitoshe aliwahi jaribu kumfikia kupitia wazazi wake lakini hajafaulu.

Mtoto mimi huzungumza naye kupitia mamake lakini ilifika wakati hashiki simu, na sasa ndio nilikuwa nataka kumuomba msamaha mbele ya wakenya milioni kumi.

Alipopigiwa simu, bi Nancy alikiri kuwa alimsamehe mumewe kitambo na kuwa hana chuki wala ubaya naye, huku akisema atarudi ila kwanza apewe muda.

Kwa upande wake Fred anasema kuwa amewacha pombe miezi saba sasa.

"Ubaya wake ni kunywa pombe na akiwa mlevi anakumbuka makosa ya zamani na anaanza vita. Sasa hapo nikaamua nimpe time apunguze pombe ili nirudi." Alisema bi Nancy.