PATANISHO: Mume Wake Ndiye Aliyenitongoza Na Nikakubali Kuwa Mke Wa Pili

Violet alituma ujumbe akisema amenyang'anywa mumewe na Bi. Rose ambaye aliwacha ndoa yake na watoto ili avuruge ya mwenzake.

"Sasa mume wangu alikuwa anatoroka kwa nyumba huku akiniambia kuwa yuko kazini lakini nikagundua kuwa huenda kwa mwanamke mwingine.

Siku moja alirudi nyumbani akiwa amebadilisha mavazi nikimuuliza anadai kuwa kuna mfanyikazi mwenzake ambaye alipata ajali na nguo zake zikapata damu, hapo ikabidi amenunua zingine.

Sasa siku nyingine anarudi na zile zile nguo alizodai kuwa zilikuwa na damu na hapo nikashuku kuwa ana mpango wa kando. Hizo tabia zake ziliendelea mpaka siku yenye alikiri kuwa ana mpango wa kando lakini akakiri atawacha. Isitoshe mwanamke yule aliwacha ndoa yake na kuja kuvuruga ndoa yetu.

Alinitumia ujumbe akisema kuwa lazima tuwe wawili kwa ndoa nipende nisipende." Alijieleza.

Alipopigiwa simu mumewe bwana Charles alikatiza mawasiliano yetu pindi tu aliposkia yuko kwenye redio lakini bi Rose alikubali kuzungumza nasi.

"Mume wake ndiye aliyenitongoza na nikakubali kuwa mke wa pili kwani alidai kuwa mkewe anamsumbua sana nyumbani kelele kila siku. Mwanaume ananishughulikia na anashughulikia Violet hata huja kwangu siku mbili kwa wiki zingine kwake.

Hata akikataa sitoki pale anafaa kukubali kuwa mimi ni mke wa pili kwani hata tayari tuna mtoto wa kijana." Alijieleza bi Rose.

&feature=youtu.be