PATANISHO: Mwanangu aliuza shamba letu sahii nakodisha nyumba

Jeff alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mamake akidai kuwa alimkosea sana.

"Tulikosana na mama 2017, tulikuwa na rafiki yangu na tulikuwa na kazi ya kuuza shamba kisha tunalewa pesa zinaisha. Mama alikuwa akinikanya na nikasema niko kwa raha zangu, hapo akakasirika na akasema atauza shamba ili nikose mahali pa kurudi." Alijitetea Jeff.

Anasema amehangaika kwani akiuza kitu chochote huwa hakidumu na masiha yake hayako sawa.

Huyu mtoto alikuwa mbaya kwani alifanya hadi nikafukuzwa kwa boma kwa ajili ya tabia zake mbaya na hadi sahii sijapata shamba. Nitamsamehe lakini akija huku asishikane na wale vijana ambao walikuwa wanampotosha.

Hata hivyo, Jeff aliomba masamaha akisema kuwa amebadilika na yuko tayari kwenda nyumbani na kufanya kila awezalo ili uhusiano wake na mamake uimarike.

Hata hivyo, Gidi alimkanya Jeff na kumuagiza ajitahidi anunue shamba ili aweze kumrudishia mamake kwa makosa aliyofanya.