PATANISHO: Nahisi kujitia kitanzi kwa sababu ya mume wangu

Mwanadada kwa jina Jane alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Reuben huku akisema anahisi kujitia kitanzi.

"Nimekuwa nikilipa nyumba kwa miaka miwili na nusu nikimsaidia mume wangu ambaye hakuwa na kazi na sasa imefika mahali ananidharau haoni kama mimi ni mtu. Sasa naskia nimechoka kabisa sijui nitafanya nini." Alisema Jane.

Wakati shida ilianza ni 2014 nilipojifungua mtoto wa pili kwani alianza kusema huyo mtoto wa pili sio wake, hata nashindwa kuelewa shida iko wapi." Aliongeza.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili kwa ndoa ya miaka tisa.

Alipopigiwa simu bwana Reuben alisema kuwa hangependa kuzungumza hewani akisema kuwa mkewe angewaleta wazazi pamoja kabla ya kuleta maneno patanisho.

Bi Jane alisema kuwa amechoka na mumewe na kuwa tayari ametoka nyumbani.

"Yangu imekuwa too much, mtoto wangu anashinda akilia akiulizia babake nitafanya nini." Aliongeza Jane akiwa na majonzi chungu nzima.