Gidi.na.Ghost.patanisho

PATANISHO: Nakupenda kuliko avocados! Tusipatie shetani nafasi

John Njoroge Kamau alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Catherine Wanjiku.

Patanisho ya leo ilianza na kicheko huku Njoroge akidai kuwa simu yake ilikuwa imeanguka chini ya kiti cha gari.

“Tumeishi na mke wangu kwa muda wa miaka 19, na tumejaliwa watoto wawili, mmoja ana miaka 18 na mwingine ana miaka 15.” Alisema Njoroge.

Ruto amtumia Kalonzo ujumbe kuunda muungano wa kisiasa

Aliongeza akidai,

Tumeishi vyema na ilifika mahali heshima ikadidimia na akadai namkosea heshima na namtusi na hapo akaondoka na kwenda kwa dadake. Imetimia miezi sita sasa tangia aondoke.”

Alipopigiwa simu bi Catherine alisema kuwa alimsamehe Njoroge ila aliamua kamwe hatorudi kwake na akamuarifu aoe mke mwingine.

“Nilikuambia nilikusamehe kitambo lakini sirudi kwako.” Alisema Catherine akidai mambo ya mahari sio makuu vile.

Duale apinga matokeo ya sensa eneo la Kaskazini, ataka server zifunguliwe!

John naye alijitetea akisema, hicho kipindi cha miezi sita nimeona maana ya mke kwani hii baridi jamani sio mchezo.

Bi Catherine naye alimuarifu John afunge ndoa na awache kukosea na kumchukulia mkewe kama kahaba.

John alimalizia akisema, “I love you more than Avocados! Hata wewe unajua napenda avocados sana sana, wacha kupatia shetani nafasi nisamehe. Nimekupea mda hata kama ni miaka miwili.”

Hatutaki vituo vya polisi Kibra, MacDonald Mariga

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments