PATANISHO: Naogopa mke wangu anaweza nyakuliwa

Bwana Austin Mukunda, 32, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Lilian, 32, ambaye walikosana mwaka mmoja uliopita.
"Vile alienda kwao alikwamilia huko na wazazi wake wanasema hadi niende kwao ndio atarudi. Sahii sina pesa kwani nina fanya biashara ya bodaboda na huwa hainipatii fedha.

Msichana aliniomba fedha za nywele na sikuwa nazo, hapo alinitishia kuwa ataondoka na kimchezo mchezo tu nilipata ameondoka." Alijitetea Austin.

Wawili wao wamekuwa kwa ndoa ya zaidi ya miaka kumi.

"Wacha niishi na wazazi kwanza nione vile watasema halafu nitakujibu." Alisema Lilian alipopigiwa simu licha ya Austin kudai kuwa amekuwa akikonda kwa kukosa mke nyumbani.

Lilian alisisitiza kuwa bado anampenda mumewe na kuwa atarudi kwake akishazungumza na wazazi na kuwa yuko tayari kungoja hadi mwezi wa sita.

Austin naye woga wake ni kuwa mkewe atanyakuliwa kwani wawili hao wameishi pamoja na wanaelewana ki tabia.

Nakupenda sana  I love you kama sweet water." Alieleza Austin.

&feature=youtu.be