PATANISHO: Nashuku Ndugu yangu alikuwa analala na mke wangu

Bwana Nabwani alituma ujumbe akiomba apatanishwe na nduguye mkuu ambaye walikosana miaka mitano iliyopita.

Kulikuwa na uvumi nyumbani kuwa ndugu yangu mkuu alikuwa amelala na mke wangu. Tukaenda nyumbani na kusuluhisha yale yote baada ya ndugu yangu kudai kuwa hamna jambo kama hilo.

Mke wake ndiye alikuwa anasisitiza kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano.

Yule mke wangu tulitengana mwaka wa 2015 na nikaoa mwingine. Tangia mwaka wa 2013 sijazungumza na ndugu yangu kwani hata kwa kongamano za nyumbani huwa hatusalimiani." Alisimulia Nabwani.

Alipopigiwa simu bwana Patty, alisema hakuwa na uhusiano wowote akidai kuwa hata kama angefanya vile ingekuwa kama laana." Sijui mbona watu walikuwa wanachochea." Alidai Patty.

&feature=youtu.be