gidi na ghost asubuhi

PATANISHO: Nasikitika Nilimuibia Tajiri Wangu Elfu Tisa

Bwana Duncan alituma ujumbe akiomba apatanishwe akidai kuwa alichukua fedha za tajiri wake.

“Kuna fedha ambazo tajiri wangu aliniwachia, elfu tisa ambazo zilikuwa za fundi alikuwa afanye kazi fulani. Nilikuwa nimefanya kazi hapo kama wiki tatu na ilikuwa imebaki wiki moja ili nilipwe mshahara.

Bibi yangu naye alinipigia simu kila wakati akidai mara ni mgonjwa mara mashemeji zake wanamsumbua. Hapo shetani akaniiingililia nitumie zile fedha ambazo niliwachia na mdosi wangu nikijua nitalipa mwisho wa mwezi.

Sasa kwenda nyumbani nikaogopa nimeharibu uhusiano na yeye kwani ni mtu ambaye ameniheshimu na ananiamini. ” Alieleza bwana Dan.

Bwana Alphonse alikiri kuwa alimsamehe Dan kitambo na kwamba hafai kushtuliwa na lolote.

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments