PATANISHO: Nasikitika sana baada ya kumpiga babangu

Nicholas, 35, alituma ujumbe wa kupatanishwa huku akisema alimkosea babake na kutorokea Nairobi na sasa imepita miaka tisa bila kurudi nyumbani.

"Ilikuwa maneno ya kugawa shamba nyumbani na mimi ndio kijana mkuu na katika harakati ya kubishana nikamchapa. Nikimpigia simu hajibu na mamangu pia hukata simu zangu." Alisema Nicholas.

Aliongeza,

Nilitaka kulima mahala nilikuwa napenda na hapo akanikataza, katika kisirani nikampiga babangu mzazi na nikatoweka."

Alipopigiwa simu, babake Nicholas alisema,

Huyo kijana alinikosea sana, mtoto mkubwa kupiga mzee wake, kwa jamii yetu hayo ni makosa makubwa na kimila hafai kukaribishwa kwa boma.

Ilifika wakati wa kugawa shamba na ilifika mahali akaamua kupiga mzee wake. Huyo mtoto mambo yake staki kuskia.

Hata hivyo mzee alisema kuwa Nicholas anapaswa arudi nyumbani, watafute wazee kisha washughulikie hayo maneno.

Mzee alikatiza mawasiliano kati yetu lakini Nicholas alikuwa na ujumbe kwa babake.

''Nimemuomba mzee wangu msamaha na naomba asinichukulie kwa ubaya."