PATANISHO: Nataka kujiua baada ya mke wangu kunipata na jirani kitandani

James, 39, alituma ujumbe akisema mke wake bi Diana, alimpata kitandani na msichana wa jirani na kuondoka kwenda kwa dadake. Alisema kuwa ameshanunua kamba ya kujitia kitanzi na tayari ameandika barua ya mwisho.

Alipopigiwa simu James alisema kuwa shetani ndiye alichangia yeye kuwa na mpango wa kando, huku akisema macho yaliona na mwili ukapenda.

Msichana ambaye alipatikana naye ni wa umri wa miaka 27 huku mkewe akiwa na miaka 31.

"Huyu msichana nimemjua kwa siku kiasi tu na si eti tulikuwa tumefanya chochote hadi iyo siku. Sikuwa najua mke wangu atarudi kwani haikuwa masaa yake ya kurudi.

Niliskia mlango umebishwa na kufungua ni yeye na nilishtuka niki wish dunia inimeze kwani hakukuwa kuzuri." Alijieleza James.

Wawili hao wana mtoto mmoja katika ndoa ya miaka saba.

Alipopigiwa simu bi Diana, alisema kuwa mumewe alimuudhi ndio maana hataki kuzungumza naye.

"Aliniudhi ndio maana staki kuongea naye, hito nishamaliza najipanga chuma yake iko kwa moto atajua mwenyewe na narudi najua kile nakuja kufanya." Alisema Diana.

Mwambie amechelewa na anafaa kuharakisha." Aliongeza akisema kuwa hiyo ilikuwa mara ya kwanza mumewe kuwa na mpango wa kando.

Alisisitiza kuwa hataki kuzungumza na mumewe huku akisisitiza kuwa ndoa yao imeisha.

Pata uhondo kamili.