PATANISHO: Ndugu wa toka nitoke wagombana vikali hewani

Bwana Elkana alituma ujumbe akiomba apatanishwe na nduguye Obed akidai kuwa alitoa madai ya kwamba aliua baba yao na tena anapanga kumuua ili abaki na shamba lao.

Alipopigiwa simu bwana Obed alidai kuwa hataki kuskia maneno ya nduguye mdogo kwani yeye huwa hasaidi familia yake ila yeye huchangiwa mke wake akiwa mgonjwa.

"Nilimpigia simu nikamwambia kuwa ndugu yako amekuwa mgonjwa sana na inafaa tumsaidie tumpeleke hospitalini." Alieleza kabla ya kumwambia nduguye kuwa hataki wawili hao waitane 'ndugu'.

Wawili hao walianza kugombana sana hewani naye Elkana akadai kuwa yuko tayari kuuza mali yake ili ahame na kuondokea matatizo hayo yote. Isitoshe alidai hataki kutambulika kama ndugu yao.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be