patanish

PATANISHO: Ndugu yangu alihepa majukumu ya kuwasaidia wazazi

Bwana Philip alituma ujumbe akiomba apatanishwe na nduguye James Odhiambo ambaye walikosana na hawazungumzi tangia alipomwambia washirikiane kusaidia wazazi.

TBT : Pata kumjua mtangazaji Jacob ‘Ghost’ Mulee Zaidi

Siku moja mzazi alinipigia simu akaniambia amepigia James ili amnunulie mbegu ya kupanda na akazungumza maneno mabaya ambayo hayakufurahisha wazazi. Alieleza James.

Nilipompigia simu na kumweleza kuwa ni jukumu letu kuwasaidia wazazi, akakasirishwa na hilo na kila ninapompigia simu kumjulia hali hajibu simu zangu. Shemeji yangu tunazungumza ila James na nataka kumuomba msamaha kama kuna vile nilimkosea.

PATANISHO: Mume wangu akilewa hutishia kuniua na nikaamua nikimbie

Sina shida na ndugu yangu na nampenda tu sana na kama kuna shida yoyote naomba tu msamaha.” Alisema James.

Aliongeza: “Wacha nisema nimebadilika sasa na kuanzia leo tutakuwa tunashirikiana na tuhakikishe tumesaidia wazazi. Tutaanza kuzungumza na hata akimaliza patanisho nitampigia simu.”

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments