PATANISHO: Ndugu yangu alinifumania na mke wake

Bwana Thomas, 38, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na nduguye bwana Duncan baada ya kumpata na mkewe nyumbani mwake na wawili hao wakazozana kabla ya mkewe kutoweka.

Bro wangu alinipata na bibi yake kwani alinipata nikiwa naye kwangu na alinipata bahati mbaya nikifanya mapenzi naye. Wawili hao wameoana kwa miaka miwili.

Thomas aliendelea,

Mke wake ndiye alikuwa amenipenda na akaja akaongea na mimi na tukaenda naye kwani hatuishi mbali. Ndugu yangu alinipata na katika ile hali ya mshtuko bibi yake akatoroka mida ya saa nne usiku.

Hapo sisi tulianza kugombana nami nikaondoka baada ya ndugu yangu kumfuata mkewe. Baada ya miezi kadhaa nilijaribu kumpigia simu kumuomba msamaha lakini hakujibu.

Thomas ambaye wakati ule alikuwa ameoa, mkewe alikuwa amesafiri na hapo akachukua fursa ile kutenda kile kitendo. Anasema kuwa nduguye na mkewe wake walitengana baada ya tukio hilo na hawakuwa wamejaliwa na mtoto.

Alipopigiwa simu bwana Duncan alisema kuwa nduguye alimkosea vibaya sana.

"Niliwapata kwa nyumba na bibi akatoka akatoroka na sijui walikuwa wanafanya naye aje kwani ilikuwa mida ya saa nne usiku." Alisema Dan akiongeza kuwa wawili hao hawajahi kuzungumza tangia siku hiyo.

Mimi hata simu yako staki, wewe wajua ulichonifanyia na hata kama ni mimi nilikufanyia hivyo hungetaka maneno yangu, ulinikosea sana. Umenifanya niwe wazimu mimi siwezi kusamehe.

Duncan bado anaumia kwa kitendo hicho na anasema hayuko tayari kumsamehe nduguye kwani bado anaumia.