patanisho

PATANISHO: Ndugu yangu alinipeleka kwa polisi nikatwangwa twangwa

Ernest Okonji alituma ujumbe akiomba apatanishwe na ndugu yake mkuu bwana Stephen, ambaye walikosana mwaka wa 2007 na hadi wa leo hawazungumzi.

Alisema kuwa walikosana juu ya mabibi zao na juhudi za wazazi wao kuwapatanisha ziligonga mwamba.

Mabibi zetu ndio walifanya tukosane vibaya sana. Kuna bibi nilikuwa naye huo wakati ikafika mahali tukakosana na akabeba vitu na kwenda kwa bibi yangu mkuu. Alisema Okonji.

PATANISHO: Babangu alitutoroka tukiwa wadogo kwa miaka 11

Aliongeza;

Alienda huko ili niende tuzungumze turudiane kwani naishi upande wa Kiambu kaunti. Nilipofika huko tukazungumza na ikashindikana kwani nilipata ameshauriwa akodishe nyumba ajikalishe.

Sasa vitu mke wangu alizokuwa ameacha kwa ndugu yangu, mke wa ndugu yangu alizuia nibebe mali yangu na ndugu yangu akadai kuwa kama nazitaka niende kwa polisi akidai kuwa najidai nina nguvu sana.

Nilipoleta polisi ndugu yangu alipigana nao huku mke wake akininyunyuzia matusi kabla yetu kupigana sana. Hapo ndugu yangu alisema kuwa niwe natembelea juu yeye akitembelea chini.

Ernest ana miaka 31 huku nduguye akiwa na umri wa miaka 41.

Alipopigiwa simu, bwana Stephen alidhibitisha kila kitu nduguye alisema.

PATANISHO: Hutaki kunirudia lakini nirudishie kitambulisho changu!

“Sikukatalia bidhaa zake kwani bibiye ndiye alisema zisitoke hapo hadi yeye azichukue. Nataka kwanza aniombe msamaha ila sio mimi nimuombe msamaha na nataka akubali hayo makosa.” Alisema.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments