PATANISHO: Ndugu yangu alitumia simu ya mzee kufuliza

Kevin alituma ujumbe akiomba apatanishwe na nduguye bwana George.

Alisimulia,

"Tulikosana na ndugu yangu Mei mwaka huu kwani kulikuwa na shida nyumbani baada ya mzee kuniambia kuwa hawana pesa za chakula. Nilikuwa na elfu moja ambayo nilipea wife akasongwe nywele, kumwambia mke wangu akasema atatuma mia tano.

Sasa mzee hana uwezo wa kutumia Mpesa na lazima mtu amsaidie. Mhudumu wa Mpesa alimwambia hana fedha na kuthibitisha ni kuwa Fuliza ilikuwa imekataa zile fedha.

Kevin anasema alipomuuliza ndugu mdogo alisema sio yeye aliyefuliza kwani hakuwa nyumbani kwa mwezi mmoja. Mhudumu wa Mpesa akasema kuwa nduguye mkuu ndiye aliyefuliza.

Alipompigia simu nduguye mkuu walikosana kwani tayari alijua mbona anapigiwa na isitoshe haikuwa mara ya kwanza.

Hata hivyo, juhudi zetu za kumfikia George hazikufua dafu kwani tayari alikuwa amezima simu yake huku Kevin akisema kuwa yeye alisema kama anataka msamaha basi anapaswa kwenda nyumbani.