pata patanisho

PATANISHO: Ndugu yangu aliwakata kata baba na mama mdogo

Bwana Vicky alituma ujumbe akiomba fursa ya kumuomba babake bwana Joel, msamaha kwa niaba ya nduguye mkuu.

Kulingana na mwanadada, nduguye yuko jela Kericho baada ya kumvamia baba na mama mdogo na kuwakatakata.

PATANISHO: Nilimfukuza bibi yangu na kuharibu kazi yake

“Sijui walikosania nini lakini ni maneno ya shamba. Sasa baba alipanda majani chai na akipata fedha anashughulikia familia yake na kusahau mama yetu, na sasa nikama jambo hilo lilimuuma.

Nikama alikuwa anasubiri watoke nje usiku wote lakini hawakutoka, asubuhi mama mdogo alipotoka ndugu yangu aliingia na kumkata baba. Mama mdogo aliposikia mayowe alikimbia na kupatana na ndugu yangu akamkata pia.” Alieleza Vicky.

Aliongeza kuwa baada ya kisa hicho, mama na baba walipona.

PATANISHO: Mke wangu hanipii furaha kwani mimi mnyama?

Bwana Joel alipopigiwa simu alisema kuwa mama mdogo bado yuko hospitalini kwani alipungukiwa na damu ila yeye yuko sawa.

Ninakuuliza, hasira yake ilikuwa ya nini na hatukuwai gombana naye? Alikuwa kwake nami nilikuwa kwangu. Yeye ndiye anapaswa kuomba msamaha kwa korti sio kwangu. Alisema bwana Joel akiongeza, hata huyo mke wake alikuwa kwa njama ya kuniua ili apate mali.

Bwana Joel alikuwa na wingi wa hasira hakumpa Vicky fursa ya kutosha kujieleza na alikatiza mawasiliano yetu mara kadhaa.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments