gidi.na.ghost

Patanisho: Ni upuzi tu! Mume afunguka kuhusu kuwa na mpango wa kando

Hivi leo katika kitengo chetu cha patanisho, bwana mmoja alifunguka na kuomba apatanishwe na mke wake kwani bado anampenda na ameacha tabia ile ya kuwa na mpango wa kando.

Bwana huyu alikosana na mke wake kwa sababu ya kuwa na mpango wa kando.

Upendo wa mama! Soma ujumbe wa Kate Actress kwa mwanawe

Jamaa huyu jina lake Ledon alisema kuwa anajuta sana kuwa na mpango wa kando kwani anampenda sana mke wake na hata wana watoto wanne pamoja naye.

Pindi tu mkewe alipopigiwa simu, Ledon alipewa nafasi ya kumwomba mke wake msamaha na kusema kuwa  hawezi rudia kosa lile tena.

”Mimi nakupenda Grace na sitarudia kukufanyia venye nilikufanyia. Ilikuwa ni upuzi tu.” Ledon alisema.

Edwin Abonyo afunguka kuhusu kuoa baada ya Joyce Laboso kuaga

Mke wake Ledon alimsamehea na kumwambia asijaribu kurudia tena kosa lile.

Wapenzi hawa waliambiana maneno matamu na kuahidi kuendelea kupendana.

 

Photo Credits: Amon Maghanga

Read More:

Comments

comments