PATANISHO: Niko na simu sita kwa nyumba nazipatianga mipango ya kando

gidnaghost
gidnaghost
Daniel alituma ujumbe akisema alikosana na mkewe Grace, juu ya mambo ya uchaguzi.

Daniel alilinganisha ndoa yake kama ya Jubilee na NASa, huku akichekesha Gidi na Ghost alipoelezea kwa urefu.

'Aki hii election hii Gidi na Ghost nimejuta sana', alisema Daniel.

Kisa na maana? Kilichotokea ni cha huzuni kwa Grace, ambaye aliarifu Gidi kwamba mumewe alikataa kuumpa pesa ya kumpelekea mtoto ushago akihofia vita ya baada ya uchaguzi.

Daniel dereva wa trela, na Grace walikorofeshana na mkewe akatoroka nyumbani. Walitofautiana kimawazo, na inasemekana kwmaba walihusisha wazazi lakini haikufaulu.

Skiza kanda ifuatayo, ujuwe kama Grace na Daniel waliweza kupatanishwa: