PATANISHO: Niliachana na mke wangu baada ya kunidanganya kwamba anaenda kazini ila hakuwa anaenda huko

Bwana Reuben aliandika apatanishwe na mke wake ambaye waliachana naye baada ya kumdanganya anaenda kazini ilhali alikuwa anaenda kwingine.
"Mke wangu alikuwa anafanya kazi lakini sikufahamu alipokuwa anafanya kazi nilipomuuliza alipokuwa anafanya kazi alikataa kabisa kuniambia

Nimekaa naye kwa mwaka mmoja, siku moja alikuja nyumbani akabeba kila kitu bila kuniarifu, baada ya siku chache niliambiwa amekodisha nyumba mahali pengine, nilipoenda hapo nilimpata mwanamume amekaa kwa kitanda

Nilimuuliza yuko wapi bibi yangu aliniambia atarudi lakini siku chache baadaye, nilisikia alienda kwa nyanya yake, sijui msimamo wake nataka kujua msimamo wake uko wapi."

Bibi yake Reuben hakupokea simu, bali bwana huyo alisema kuwa alipompigia simu alimpa matusi huku akimtusi na mama yake mzazi.