PATANISHO: Niliambiwa hakuna hata paka itakayopelekwa kwetu

gidi.na.ghost
gidi.na.ghost
Mark, 30 alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Josephine, 25, akidai angependa kusaidiwa kurejesha uhusiano kati yao.

"Tulikosana mwaka wa 2018. Sasa huyu msichana vile nilimuoa kutoka kwa mamake wa kambo na tukaja tukaishi naye na tukapata mtoto. Baada ya siku kadhaa mtoto akaaga." Alisimulia Mark.

Sasa mamake mzazi ambaye alimtenga akiwa na mwaka mmoja ndiye alipiga simu akidai anataka kuzungumza na mke wangu. Mke wangu sasa alimtambua na kumkubali kama mzazi na hapo akaamua kumfuata."

Mark anasema wawili hao huzungumza lakini kila wanapopanga kukutana au kurudiana, Josephine husongeza masiku.

Wawili hao walikuwa wameishi kwa ndoa ya miaka minne.

Huyo mwanaume nikiwa naye aliniambia yuko na miaka 19 na ukimwangalia ni mtu mzima, nikamwambia aniambie miaka ya ukweli. Miaka mitatu sikujua miaka ya ukweli.

Halafu kuharibu mambo, nimeoneshwa madharau chungu nzima. Huyu mwanaume alichukua gazeti alikata kunichoma nywele, baada ya mtoto kufariki alinisingizia kuwa nimemuua. Alijitetea Josephine akidai kuwa shemeji yake alimwambia kuwa hakuna hata pussy itakayoenda kwetu.

Josephine alipopewa fursa alimwambia Mark kuwa alikuwa na hamu sana ya kuishi naye lakini madharau yake ndiyo yaliharibu kila kitu.

"Aliniambia hataki jeneza kwake na nikamwambia kuwa ni sawa nitarudi kwetu. Siwezi rudi kule kwani babangu mzazi aliniambia nisiwahi rudi kwake na sasa ameaga dunia." Josephine alisema.

Alisisitiza kuwa alikuwa anampenda Mark na kilichofanya watengane ni madharau huku akidai amewachana na mambo ya wanawake na anashughulikia kazi yake.