patanisho

PATANISHO: niliangukia mume ambaye hakuwa anasoma katiba

Eunice,25, kutoka Teso alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Ronald.

“Yeye alikuwa anataka niishi nyumbani naye mjini ila hataki niende mjini. Kisha nikaskia fununu kuwa analeta wanawake kwa nyumba ila mimi naishi nyumbani na wazazi wake.” Alisema Eunice.

PATANISHO: Nilimvulia mume wangu nguo baada ya kumtusi mama

Eunice anasema baada ya kutoka kwake, alipendana na mwanaume mwingine na kwa bahati mbaya alipata mwanaume ambaye wanalala kitandani pamoja kama wanawake wawili kwani hawasomi katiba.

Alisema wazi kuwa ana miss katiba ya bwanake na anampenda sana.

Kabla ya kutengana kwao wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka miwili unusu na walijaliwa mtoto mmoja na alipopigiwa simu bwana Ronald alisema kuwa atafanya maamuzi kivyake kisha atamjulisha mkewe.

PATANISHO: Kondoo ndio ilitutenganisha na mke wangu

“Kurudi sio tatizo lakini tatizo ni kuwa alishaolewa yeye kwani mke wa mtu akikurejelea sio jambo nzuri. Ninacho kifahamu ni kuwa bado yuko kwa bwanake.” Alisema Ronald.

Bwana Ronald naye alisema kuwa tayari ana mke na amejaliwa na mtoto na hangependa Eunice aondoke kwa ndoa yake ili amrudie na pia hangependa kuwa na wake wawili.

Upande wake Eunice, alikubali uamuzi wa Ronald na ameamua kuendelea na maisha yake na kutafuta mpenzi mwingine.

Patanisho: Amekuwa mkali kama simba ninapoitisha tendo la ndoa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments