PATANISHO: Nilianza Kuonja Kando Kwani Niliogopa Mke Wangu Ataniambukiza Magonjwa

patanisho 1
patanisho 1
Reuben mwenye umri wa miaka 39, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama watoto, Sophia Nkatha.

Kulingana naye, kiini cha wawili hao ambao wameoana kwa miaka kumi na mitano kukosana, ni kuwa yeye ndiye aliyekuwa na tabia zake za mipango ya kando.

"Gidi Nlikuwa na tabia za ufisi na nikaanza kulamba lamba nje." alieleza Reuben.

Bibi yangu alikuwa na shida fulani kwa miezi kama mitatu ivi na nilipomueleza aelekee hospitalini kutibiwa alikataa na hapo nikaamua kwenda hospitalini kueleza shida zake.

Hapo nikapewa madawa na nilipomletea dawa akakataa kunywa zile dawa. Hofu yangu kuu ilikuwa labda tungeambukizana magonjwa ikifika ni hali ya kufanya mapenzi." Alijieleza zaidi huku akidai kuwa wawili hao wamejaliwa watoto watatu.

Alipopigiwa simu Bi Sophie 35, alikiri kuwa hataki kuskia chochote kuhusu bwana Reuben na akakatiza mawasiliano Kati yetu.

"Mimi nahisi bado tu nampenda zaidi na sasa naona watoto watateseka endapo nitaamua kuoa mke mwingine. Imagine nilienda kando kwa ajili yake kwani nilimpea dawa na akakataa. Aliongeza Reuben asijue la kufanya.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be