PATANISHO: Niligundua Kuwa Mke Wangu Aliingia Kwa Ndoa Akiwa Mja Mzito

Alex alituma ujumbe akiomba ndoa yake ya miaka minne iokolewe kwani inasambaratika.

"Tulikosana na mke wangu mwezi wa Novemba mwaka uliopita. Shida ilitokea wakati tulianza kukorofishana na nyanyake.

Nilimuoa mke wangu na mtoto mmoja kisha nikaja kugundua kuwa aliingia kwa ndoa akiwa na mimba. Nikakubali na nikamweleza kuwa nitamshughulikia mtoto.

Mtoto mmoja aliwachwa kule mashambani na hapo nyanya yangu alianza kutumia fursa ile kama biashara akidai kuwa nafaa kumtumia kama shilingi elfu moja mia tano kila wiki.

Nilipokasirika nyanyangu akanitishia kuwa atampeleka mke wangu kwa wanaume wataomshughulikia." Alielezea Alex.

Alipopigiwa simu bi Helen alidai kuwa hataki maneno yake kwani shemeji wake walimfanyia mambo makubwa.

Mojawapo ya mambo hayo ni kugombana na nyanyake Alex na pia kupigwa na bwanake.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be