Patanisho: Niliharibu ndoa ya kijana wangu baada ya kuenda kwa mganga

ghostansgidifri
ghostansgidifri
Ni miaka kumi tangu huyu baba na kijana wake wawasiliane.

Kisa na maana?

Alienda kwa mganga ampatie dawa aweke kwa chakula lakini huyo kijana akagundua.

Bwana  John alimwelezea Gidi kwa ufupi

 'tumekosana for so many years, sasa katika hiyo harakati ya kujaribu angalau tuongee na yeye imenishinda so rafiki yangu akaniambia tumia njia ingine akanielekeza kwa mganga. Nikatoa hiyo dawa nikapea bib ya kijana wangu. Unajua sasa lazima utafute mtu akokaribu na yeye nikampea akajaribu kumwekea na kijana akanotice. Sasa hiyo ikafanya tukakosana. 

Mzee amesononeka sana kwasababu huyo kijana wamekosana na bibi yake.

'Ehe aligundua niliambia bibi yake aweke dawa kwa chakula yake' aliongeza Mzee John.

Na hii dawa ingechangia nini?

Ni ile tuu niliambiwa eti itaweza kumbadilisha kwa njia moja iweze kubadilisha na aweze kurudi nyumbani. 

Na walikuwa wamekosana na huyo kijana?

Mama yake alikufa sasa nikaoa mke mwingine. Kuoa mwingine sasa ndio wakakosana yani pia yeye alijaribu kumwuua. hawakuwa wanaskizana.'

Mbona ma wa kambo alikuwa anataka kumwuua huyu kijana?

John alisema, ' Alijaribu kabisa akamwekea dawa na si mara moja na kijana alikuwa akiwekwewa. Sasa kuna vile sikjui kijana alijua vipi, sasa akatoroka nyumbani na kasema hatawahi rudi'.

Alihimiza Gidi aweze kumpigia simu kijana wake, washirikiane huku akisema'

unajua kunawakati tulijaribu kuskizana na yeye lakini kwa vile alikuwa tumejaribu kumwuua akaniambia kama unataka mtu aahidi mali yako basi nenda ukanunua mtoto. Sasa tafadhali hiyo imenichanganya lakini hata hivyo nilimpita mpaka kuharibu ndoa yake 

Doh!

Mke wake kwa sasa alifukuzwa nyumbani na mvulana anayeitwa Mike.

Kwa bahati mbaya Gidi hakuweza kumpata Mike kupitia simu na wakaamuua wapigie bibi ya kijana.