PATANISHO: Nilikuwa nakaa kwa bwana yangu kwa ajili ya watoto wangu si mume

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Katika kitengo cha patanisho hii leo bwana Godfrey Okumu,50 alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake Beatrice,50, ambaye anakataa kuenda mashambani huku akidai kuwa lazima watoto wake wamalize shule.
"Nilitoka Nairobi Machi mwaka huu nikaenda mashambani alafu corona ikaripotiwa nilirudi Nairobi tena nikamwambia kuwa anapaswa tuende mashambani naye akakataa

Mke wangu anafanya hayo kwa maana ako na pesa tulilipwa  kwa maana tulikuwa na kesi kortini, nilimuuliza pesa ziko wapi aliniambia ameweka kwe benki na zilizobaki anaweka kwa ajili ya karo ya shule

Sitaki kuoa mke mwingine ilhali nataka arudi nyumbani." Alieza Okumu.

Mkewe Okumu naye alikuwa na haya ya kusema,

"Anataka turudi nyumbani na hana chochote analishwa na mama yake, nina watoto wa kidato cha kwanza mimi ni mama mzima siwezi enda kulishwa na mama mkwe

Ako na watoto ambao si wangu lakini na walea, nyumbani hatujajipanga." Alizungumza Beatrice

Bwana Okumu alisema kuwa amechoshwa na Nairobi na mke wake anapaswa kutumia pesa alizonazo kama nauli, ilhali Beatrice alisema kuwa amepitia mengi katika ndoa yake na alikuwa katika ndoa yake kwa ajili ya watoto wake na mumewe.

Beatrice alimaliza na kusemaa kuwa mumewe anapaswa kumtumia nauli aweze kuenda nyumbani.