PATANISHO: Nilikuwa nalala na kisu kitandani kwa raha zangu

patanisho.
patanisho.
Hared ndiye aliyeomba apatanishwe hii leo na mkewe, bi Queen, akisema kuwa ndoa yake imeharibika.
"Tulikosana na mama watoto na akaenda kwao lakini alienda kwa dadake mkubwa mwenye alikuwa mja mzito. Mimi kwenda Huko akaniambia hataki kazi ya bwana na ana watoto wawili kwa hivyo ningoje wafikishe umri wa miaka 18 na sijui nitafanyaje." alieleza bwana Hared.

Kulingana na bwana huyu wawili mkewe alikuwa anapokea simu kutoka kwa wanaume anaoamini ni wapenzi wake.

Saa saba watu wanafaa kulala lakini jamaa wanampigia simu. Tuliketi chini tukazungumza lakini baada ya siku tatu bado alirejelea ile tabia.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitatu na wana watoto wawili.

Queen ambaye ni shabiki wa redio Jambo alipigwa simu alisema hataki mambo ya wanaume.

"Lakini hayo maneno anasema hayo ni yake. Nimejaribu lakini sioni kama anataka kuishi na mimi. Nilipotoka kwake alikuja kwa ploti na kunitusi, nimemwambia atafute msichana mwingine waishi naye" Alisimulia Queen.

Isitoshe anasema Hared alimuita kahaba na kuwa mamake ni kahaba pia.

Isitoshe mumewe alikuwa analala na kisu akimtishia kumuua na kumfanya kiwete.

Hiyo kisu unasema ni yangu tu ya starehe ya kula paipai. " Alijitetea Hared.

Licha ya hayo yote bi Queen alisema kuwa roho yake imekataa kurudiana na huyo mume.