rjpatanisho

Patanisho: Nililala kwa sitting room baada ya mke wangu kugeuka kwa kitanda akaface upside down

Chanzo cha ugomvi kati ya wapendwa wawili huwa mambo ya mapenzi pale nyumbani.

Katika kitengo cha Patanisho Michael amejaa wasiwasi baada ya mke wake kukata kurudi nyumbani, baada ya sherehe za Krismasi.

Amejaribu kumshawishi arudi lakini mke amekataa. Kisa na maana?

‘ni ile ya kubishana kidogo lakini si ile ya kukosana kabisa, sababu tunabbishana asubhi tunarekebisha usiku.’

Kumbe sasa yeye alichukulia serious akaiweka kwa roho yake ikawa tuu anagrow serious mpaka akaamua kuenda na krismas. 

Je wakati mke aliondoka kuenda ushago krismas alisema aliondoka akisema amechoka na yeye na hatarudi?

‘No alisema anataka kuenda nyumbani aone watoto sababu walikuwa wameenda kutembelea nyanya yao huko, sasa akasema anaemda kusherekea na arudi na watoto waendelee na shule. Hiyo ndio inanipee wasiwasi. 

Na akijaribu kumshawishi anasema nini?

‘Anasema atarudi lakini hajui lini, ananiambia tuu yeye atajua.’

Walikoseana mambo ya mapenzi? Alikuwa anajaribu kumshawishi washiriki kimapenzi lakini mke wake ni kama hakuwa anataka, hata wakati moja alilala upside down

Michael wa miaka 29 anaomba patanisho katika yake na mke haraka waweze kuridisha uhusiano.

Liz, mke wake wa miaka sita,  kwa bahati mbaya alikuwa mteja an ilibidi Gidi ajaribu kumpata mara nyingi.

Liz alikuwa akiskiza Radio Jambo na laiwasha simu huku akiarifu Gidi kwamba ni kweli ni mambo ya kimapenzi.

Alifanya nini?

‘Tulikuwa tumekosana tuu mambo ya nyumba, akaniambia nipack niende kwetu, na hakurudi alirudi majioni hivi na sikuwa na pesa, nikasema wacha tuu nitulie, juu hiyo siku ndio alitangulia kulala kwa sitting room, na mimi nikalala kwa kitanda,

sa yeye venye alikuja saa nane usiku, mimi nikapinduka coz saa ngapi hizo anakuja kwa bed? Sio mara ya kwanza kuniambia nipack niende kwetu, ni kama mara tatu. Sitaki kusikia mambo yake Tafadhali Gidi usiniunganishe na yeye coz ata nilimwabia nitakuja akaniambia atachoma nguo za watot zenye zimebaki huko. na nikamwabia achome zote akitaka.  

Liz hakutaka kuongea kwa simu na Michael, na Gidi akamshawishi aende kwao nyumbani ajaribu kuongea na yeye juu ya hiyo hasira.

Skiza kanda;

 

 

 

 

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments