PATANISHO: Nilimchapa mwanamume niliyempata na mke wangu hadi kumkata vidole

Katika kipindi cha patanisho, mwanamume mmoja alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe waliokosana mwaka wa 2014 baada ya kumpata mkewe na mume mwingine kisha kumchapa na kumfukuza.

Bwana David Andai alikuwa na haya ya kueleza,

"Siku moja nilitoka nyumbani nikaenda kazini lakini mke wangu hakujua kama sikwenda kazini, niliporudi kutoka kwa ziara zangu nilimpata mke wangu akiwa kwa jirani na mwanamume mwingine

Alikuwa amemuacha mwanangu akiwa na miezi sita akiwa hajakula na akiwa nje na watoto wengine, jamaa huyo aliyekuwa naye alikuwa amekuja kwa mjomba wake

Nilikasirika mpaka nikamchapa mwanamume aliyekuwa naye hadi kumkata kidole pia nilimchapa mke wangu na akatoroka akaenda kwao."

David alisema kuwa alikubali makosa yake kwa kumchapa mkewe na kuwa amemsamehe mke wake, alikiri kuwa alikuwa anampenda mke wake sana.

Je unaweza mpa Bwana David ushauri upi? kwa mengi zaidi tembelea mitandao ya kijamii ya youtube.