PATANISHO: Nilimchoma Bwanangu Na Mafuta Taa Kwa Upendo Tuu

Mildred 28, alituma ujumbe akiomba apatanishwe kwani alihisi kuwa ndoa kati yake na bwanake Robert mwenye miaka 30, inasambaratika kadri na upendo au juhudi zake.

"Mume wangu tulipatana 2010 na tumekuwa pamoja miaka saba. Mimi ni Mluhya naye Mkalenjin na baada ya mamake kuskia kabila langu alipinga ndoa ile huku akidai kuwa wa Luhya wanatoka Uganda na hataki.

Pamoja tuna mtoto mmoja lakini nina mmoja ambaye niliingia naye kwa ndoa na alianza swala la kunipiga huku mtoto akiwa na miezi minne pekee." Alijieleza Mildred akidai kuwa amekuwa akiona jinsi alivyokuwa na tabia ya kutongoza wanawake katika mtandao wa Facebook huku siku moja akimweleza mmoja wao kuwa amemwacha Mildred na angetaka kumuoa.

Kulingana na bwana Robert ambaye hakuwa ameonekana kwake nyumbani kwa mda wa siku tatu, alisema kuwa alikuwa ameelekea Nairobi kutafuta kazi huku akifichua kuwa mke wake alianza tabia zisizoeleweka, kwani kuna siku aliwahi mwagilia mafuta taa na basi alishuku nia yake ni kumuua akiwa usingizini.

"Mke wangua mwenye tabia ya kupigia nambari anazopata kwa simu yangu siku moja alipiga simu ikawa ni mwajiri wangu, hapo mwajiri alikasirishwa na maneno yale na hapo nikafutwa kazi. Hata amepigia wengine na kila mara napoteza kazi zangu." Alisema Robert.

La kushangaza ni kuwa Midred alikubali alikosea kwa kumchoma mumewe na mafuta ya taa huku akidai "Ni kwa upendo tuu kwani ana tabia za wanawake na hanishughulikie."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be