PATANISHO: Nilimchoma Mke Wangu Na Heater Kwa Shingo

Machero alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Jennifer ambaye walikosana mwezi wa Februari tarehe kumi na sita mwaka huu na kumuachia watoto.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na tatu na wamejaliwa watoto wawili. Machero ana miaka 35, mkewe Jennifer ana miaka 31.

"Sijui shida ni ipi lakini nashuku ni ile hali yake kutafuta jinsi tutakavyoachana. Sasa siku moja tukakosana na akatokana nguo zote akidai ameelekea kufulia kwa mdosi wake, lakini akaziwacha kwa rafiki yake." Alijieleza Machero.

Sasa aliporudi tukaanza ugomvi kidogo kidogo na kwa bahati mbaya kulikuwa na heater inachemsha maji na hapo nikamchoma kwa shingo na akapata jeraha, ila haikuwa kupenda kwangu. Baada ya hapo aliondoka bila kuchukua watoto lakini naskia anaishi maeneo ya Kawangware." Aliongeza.

Kulingana na Machero anashuku kuwa yote yalianza baada yake kupoteza kazi mwaka wa 2012.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be