patanish

PATANISHO: Nilimfukuza bibi yangu na kuharibu kazi yake

Ni kipindi ambacho kimekuwa kikiwapatanisha wapenzi na pia wanaume na wake zao iwapo wameweza kukusona,mwanaume mmoja aliweza kutuma ujumbe ili aweze kupatanishwa na mke wake kabla aweze kujiua baada ya kumfukuza nyumbani kwao.

PATANISHO: Mume wangu hata nguo za ndani hanishughulikii

“Nilimtafutia mke wangu kazi ya kaunti baada ya kumtafutia alianza kuja nyumbani akiwa amechelewa,

“Nilihisi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wenzake ambao wanfanya kazi na wao,nikimuuliza hakuwa ananijibu kwa maana mke wangu ni kichwa ngumu,” Alieleza Joash.

51448053_623797368060114_5792303046332895467_n(2)

Haikuchukua muda bali aliweza kuenda kumtafuta aliyekuwa akimshuku ana uhusiano wa kimapenzi na mke wake Lucy na watu wa pikipiki ili kumuuliza maswali na kumchunguza bali hakuweza kumpata.

“Nilienda nikaharibu kazi yake nikasema afutwe kazi kwa sasa anangoja mshahara pekee hataweza kurudi kazi,

“Wiki jana aliweza niambia ameenda mazishi nikapiga simu kwao nikaambiwa hakuna mazishi aliporudi baada ya siku mbili nilimwambia arudi alikokuwa ametoka,

“Baadaye niliweza kuambia alikuwa mazishi kwa nyanya yake,” Alisimulia Joash akiwa ana juta.

PATANISHO: Mke wangu hanipii furaha kwani mimi mnyama?

Mke wake alisema kuwa hakuweza kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na wanaume wa kazi yake.

“Baby nakuomba msamaha kwa yote nimefanya,nimeweza kubadilika ata ukikija utapata nimebadilika,

“Nimeamua moyoni mwangu nibadilike tuweze kurudiana wakati umeenda sana tafadhali naomba msamaha,”Alizungumza Joash.

PATANISHO: Ndugu yangu alinipeleka kwa polisi nikatwangwa twangwa

Mke wake hakuweza kukubaliana na maneno yake bali aliweza kumpa dada yake simu ili aweze kuongea kwa niaba yake.

“Tumechoka na mwanaume huyo nitamtafutia dada yangu mwanaume wingine ambaye atampa heshima na kumtambua kuwa yeye ni mwanamke,

“Tumeona visa vingi mwanamke anauwa na mume wake,kwa hivo sitaki dada yangu apitie hayo,

“Kwa hivo Joash aendelee na maisha yake,kwa maana kabla ya kuolewa nitahakikisha dadayangu ameolewa na mwanaume mzuri,” Alizungumza dada yake Lucy.

Photo Credits: Instagram

Read More:

Comments

comments