ghost son

PATANISHO: Nilimfumania Mke Wangu Akibugia Chang’aa Na Mpango Wa Kando

Patrick alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Fidelia ambaye walikosana sana takriban miezi mitano iliyopita.

“Mimi nilikosana na mke wangu kwani nilimpata na jamaa fulani wakinywa chang’aa maeneo ya Likoni, mwezi wa pili mwaka huu. Tumeishi naye kwa mda wa miaka kumi na mitano na tumejaliwa watoto watano, mmoja akaaga dunia sasa wamebaki wanne.

“I Was A Chang’aa Taster At 14!”, Reveals Ghost Mulee

Tukizungumza sasa hivi mke wangu yumo Nairobi lakini tumekuwa tukiwasiliana lakini mara nyingi hupiga simu kujulia watoto hali.” Alijieleza Patrick.

Patrick ana umri wa miaka 45 huku mkewe akiwa na zaidi ya miaka thelathini.

Alipopigiwa simu bi Fidelia alijitetea akidai kuwa hakutoweka kwa ubaya kwani shida ilikuwa karo. “Mume wangu hakuwa anawajibika na karo ya watoto kwa hivyo ilibidi nitoke ili niwashughilikie kivyangu. Isitoshe akiwa na fedha mimi sio mwanamke juzi aliuza ndama na akaleta mwanamke mwingine kwa nyumba.” Alijitetea kabla ya wawili hao kuanza ugomvi mkuu na kukosa kuelewana.

PATANISHO: Annette Amsamehe Wycliffe Mwenye Tabia Ya kubugia Chang’aa

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments