PATANISHO: Nilimfumania Mke Wangu Na Ndugu Yangu

Wamae mwenye umri wa miaka 29, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na aliyekuwa mkewe Jane mwenye umri wa miaka 24.

Kulingana na jamaa huyu walikosana mwaka wa 2015 na tangia siku hiyo wawili hao hawajawahi zungumza hata siku moja baada ya 'kunikosea vibaya sana.'

"Mimi nafanya kazi Ol Karao ya butchery na siku moja nilimuacha mke wangu nyumbani kwa ajili ya kazi, kwa hivyo nilikuwa narudi nyumbani kila baada ya wiki moja. Basi siku moja nikapata ujumbe kuwa bibi yangu ana uhusiano na ndugu yangu mdogo." Alieleza Wamae.

Gidi sikuamini kwani mke wangu nilikuwa nimemtoa kanisani. Sikuamini kwani nikaamua kuchunguza kivyangu. Basi siku moja nikarudi nyumbani bila kueleza nasafiri nikarudi saa nne ya usiku, nikapata wamezima taa na mke wangu aliposkia nikibisha mlango akatoka haraka akaketi kwa kiti pamoja na ndugu yangu huku wakijifanya wanacheza na simu kwa giza. Mimi niliwaamrisha kutoa manguo na nikaita mama wangu na ndugu zangu nikawaamrisha watoke uchi wa mnyama. Nilikuwa niwafanyie tendo la kinyama lakini niliondoka nikaenda zangu."

Aliongeza wamae huku akidai baada ya hiyo siku hajazungumza na yeyote kati ya ndugu yake na mke wake kwani hata mamake hajazungumza naye.

Alipopigiwa simu bi Jane, alidai kuwa ameishi akimtafuta mumewe kwa miaka hiyo yote bila mafanikio.

"Sasa ningemfukuza ndugu yako? Ulitupata uchi kweli? Wacha uwongo kwani nawezaje lala na ndugu yako?." Aliuliza Jane.

"Sasa sina ubaya na wewe, hayo yote yalikuwa urongo tu kwani tulikuwa tu kwenye kiti na hatukuwa tumelala." Alieleza Jane kabla ya bwana Wame kububujikwa na machozi akose la kusema.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be