PATANISHO: Nilimpenda Mke Wangu Hata Baada Ya Kuniambukiza Maradhi

Chris Alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama mkwe akidai ndoa yake ipo mashakani.

Tulikosana naye kwa mda wa miezi mitatu iliyopita. Mimi makosa yangu ni kuwa nilikuwa nafanya kazi ya jua kali na mke wangu alikuwa anataka nimtafutie kazi wakati tulikuwa tunaishia Bungoma.

Nilimpigia simu nilipofika Nairobi na hakuwa anajibu na kumbe alikuja akashikana na kijana wa kinyozi. Nilimpata na mtoto mmoja nami nikaingia kwa ndoa na mtoto mmoja.

Nilimpata na ugonjwa nami nikaadhirika na nikaamua kumpenda na kuishi naye kwa miaka saba bila shida yoyote. Sasa yule kijana aliposhika simu nikamueleza ukweli wa mambo na nikamwambia aanze kumeza madawa.

Sasa aliporudi kwa hasira nikampiga na akaondoka na kurudi nyumbani. Mama mkwe naye nilimtumia ujumbe mbaya wakati mke wangu alikataa kushika simu zangu.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be