PATANISHO: Nilimpiga mke wangu hadi nikamvunja mkono

Alex Jumba, 32, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Mary, 31, baada ya kumpiga hadi kumvunja mkono, huku akidai kuwa anahuzunika sana kwani bado anampenda. Kinaya kikuu!

"Kuna vile kazi yangu iliisha na mwaka mzima yeye ndiye alisimamia maneno ya kulipia nyumba. Kuna siku alinitusi akiniambia maneno ya kazi.

Kuna bag ilikuwa hapa na rafiki yangu aliomba ile bag kwani ilikuwa na kitambulisho changu. Siwezi pata yoyote kwani kila ninapoenda wanaitisha kitambulisho." Alieleza Alex akisisitiza mkewe alimuongelesha vibaya.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya mwaka mmoja tu na walipotengana mkewe alienda kwao nyumbani.

Alex alimuoa Mary akiwa na watoto watatu lakini wawili hao bado hawajafanikiwa na mtoto pamoja.

Nilikuwa nimeingia katika biashara ya pikipiki lakini unajua ukiwa mgeni wateja wanakuogopa so kazi haijashika bado." Aliongeza Alex.

Alipopigiwa simu bi Njeri alisema kuwa walikuwa wamegombana kidogo na wakakosana.

"Mimi nimekusamehea lakini siwezi rudiana nawe." Alisema Njeri huku akishikilia msimamo wake kuwa kamwe hatorudiana na Alex.

"Anipe mda kwanza nifikirie kwani bado sijamtema kabisa. Imagine tuligombana na nilipotaka kwenda alishika mkono na kuuvunja, isitoshe akachukua chuma na kunipiga nayo" Aliongeza Njeri huku akimpa Alex matumaini.

&feature=youtu.be