PATANISHO: Nilimtusi bwanangu nikamwabia nina wanaume wengi

Katika kitengo cha patanisho, mtangazaji Gidi alipigwa na butwaa baada ya mwanadada Susan kumuarifu anataka kuptatanishwa kabla afe.

Bi Susan alishtua Gidi vile aliandika SMS yake ya kuomba patanisho. Kisa na maana? Susan anampenda bwanake na mpenzi wake hamwongeleshi. Anafikiria mambo mengi kwa sasa.

Shida ilianza wakti mwanaume mwingine alipigia Susan simu ambaye hakushika hiyo simu.

Kwanini? 'Alikuwa tuu mtu was kunisumbua'. Amesave numba yake kama 'mtu wa kusumbua sumbua'.

Huyo mtu Susan anadai ni customer anyempigia simu mara kwa mara ampelekee chakula maana anafanya kazi kwa hotel.

'Nilikuwa na yeye Sunday na mwanaume mwingine akanipigia, na sikushika hiyo simyu na bwanagu anakakasirika. Ni mtu namjua lakini ni sumbua. Ni customer wetu pahali nafanya job, na ni kwa hoteli na akihitaji chakula nampelekea. Anafikiria kunitongoza. Lakini sikuongea na yeye'.

Susan anamiaka 25 na mumewe na miaka 34. Hawaishi pamoja kwasababu Susan ni mke wa pili.

'Saa hi ameniblacklist, na ako na simu yangu na nikaipasua. Bwnagu alienda na simu yangu na kwa sas nataka anirudishie niende zangu'.

Tulikosana wiki iliyopita sasa nikakasirika nikapasua simu yangu, sasa ikaharibika, akaichukuwa atengeneze, nilimtusi, na saa huu ameblacklist numba yangu. Nataka kuomba msamaha'.

Huyu mwanadada alikufa mwoyo wakti Gidi alikosa kumpata bwanake Wellington kupitia simu.

Labda hakuwa anataka kuongea na Gidi, iliwapate suluhisho. Kulinganga na Gidi, labda bi Susan ni mpango wa kando kwani hajawahi pelekwa nyumbani kuonanan na wazazi na pia wawili hawa hawana mpango wa kupata watoto. Isitoshe, Susan hamjui bibi wa kwanza.

Wanajambo walimpatia Susan ushauri wakisema Susan asahau uhusiano na Wellington kwasababu labda huenda kuna wanadada ambao wako kwa uhusiano, na wanaume wakijidanganya kwamba hao ni wake wa pili ilhali hao tuu ni mipango ya kando.