PATANISHO: Nilimvulia mume wangu nguo baada ya kumtusi mama

Mama Ravien aliomba apatanishwe na mumewe bwana Ronald ambao walikosana wakati wa likizo ya pasaka akidai kuwa mumewe alimtusi mamake na hapo akamvulia nguo.

"Ilikuwa good Friday na kwa nyumba hakukuwa na kitu akaniambia mwenzangu hatuna kitu na nikamwambia kuwa nitapigia mamangu atutumie kitu. Kumpigia mamangu akasema sisi ndio tunafaa kumtumia kitu na kumbe hayo maneno yalimkwaza bwanangu." Alisimulia.

"Mwezi wa tano alienda kunywa pombe na aliporudi akalalamika kuwa sijapika licha yake kutowacha fedha, akachukua fedha zangu na kuniambia nipelekee mamangu mjinga, malaya ambaye hatumii akili.

Alieleza kuwa bwanake pia alimshika shingo na kumnyonga, baada ya mda mfupi akamtusi huku akimtusi na kwa hasira mama Ravien akamvulia nguo.

Kesho yake asubuhi mamake alinipigia kuniambia kuwa bwanangu ameenda nyumbani. Nataka kujua msimamo wake kwani hata watoto hajashughulikia.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne na wana mtoto mmoja baada ya kujuana mwaka wa 2010.

Alipopigiwa simu bwana Ronald alisema kuwa wawili hao walizungumza na kila kitu kikaisha huku akishindwa mbona mkewe alimtafuta kupitia Radio Jambo.

Ronald alisema, "Mimi huzungumza na huyu mwanamke kila wakati na tena ananishangaza amenileta Radio Jambo na sisi huzungumza."

Alisema kuwa atarudi nyumbani mwisho wa mwezi.

Isitoshe mkewe alisema kuwa kuna siku alilewa na huko kwa bar akaambiwa kuwa mwanamke wa Busia sio mwanamke kwani yeye ametoka Kakamega.

&t=333s