PATANISHO: Nilimwambia Mke Wangu Ananuka na haogi

Hapo jana, Peter alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe, Rose Akinyi.

Kulingana na bwana Peter 26, walikosana mwaka uliopita kwani alikuwa na tabia za matusi, madharau na kumpiga na baada ya mkeo kuchoka alianza kulipiza kisasi kwani yale yale aliyomfanyia ndiyo aliyofanyiwa.

"Ilifika siku moja nikamueleza kuwa haogi ananuka na jambo hilo lilimkasirisha sana kwani ninapomuomba msamaha hunikumbusha neno hilo na ana wingi wa hasira sana. Ilikuwa tu katika hali ya hasira kwa nyumba." Alijieleza bwana Peter akiongeza kuwa amekuwa akishughulikia mtoto wake ambae wanaishi na mkewe upande wa Nairobi.

"Tulipopata mtoto naye, tulikuwa tunapendana na baada ya mtoto akaanza madharau akaanza kutembea tembea na wasichana wa kazini kwake pia na wakubwa wake huku wasichana wale wakaanza kunisumbua. Tukahamia Isinya akaendelea na zile tu tabia na hapo nikachoshwa naye na hapo akaanza kunishuku kuwa naenda nje ya ndoa na mimi sikuwa nahanya. Alianza kunishuku na mfanyikazi wangu na siku moja jamaa flani alinisalimia na marafiki zake wakamueleza, aliporudi nyumbani alirudi kama amenirushia mangumi bila sababu lolote. Sasa naendelea maisha yangu na mtoto." Alijieleza bi Akinyi akiongeza kuwa bwanake hashughulikii familia yake kwa lolote lile.

"We oa wasichana ni wengi mimi nimekuwachilia sikusamehei juu ungekuwa mtu anaonesha utu ningekusamehe lakini wewe bado ni ule ule." Aliongeza Akinyi mwenye umri wa miaka 23.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be