PATANISHO: Nilioa mwanadada mwenye watoto wawili nikiwa 16

Bwana Kereinya kutoka Meru ndiye aliyeomba kupatanishwa na mkewe bi Wangari, akidai kuwa aliondoka na kumtenga mwaka wa 2018 akiwa kazini na hadi wa leo hajawahi regea nyumbani.

Kereinya aliomba usaidizi ili mkewe aregee na waendeleze maisha yao.

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka saba na alimuoa na watoto wawili ila wao hawakujaliwa na mtoto pamoja. Cha kushangaza ni kuwa jamaa huyu ni wa miaka 23 na mkewe ana miaka 32.

"Hata kama amechukuliwa nataka tu anipe neno la mwisho nijipange." Alisema.

Nilitoka nyumbani kuelekea kazini na tulikuwa tumegombania mia tano na akatishia ataondoka, hapo nikamwambia nitaomba fedha na kumtumia. Nilipomtumia naye akaona hizo ndio nauli na akaamua kuondoka.

Anasema kuwa alijaribu kumpigia simu hii leo ila dadake ndiye aliyejibu simu. Lengo lake ni kutaka tu kujua anachotaka.

Nimekuwa nikijipanga kwenda kwao ila nafanya kazi ya mchina na ni ngumu sana.

Alipopigiwa simu, dadake Wangari, bi Rebecca ndiye aliyejibu simu yake akidai kuwa dadake yuko kazini. Alisema kuwa simu yake imeharibika ila laini yake ya simu iko kwa simu yake.

"Wangari aliniambia walikuwa wameongea na akamwambia hawezi rudi kwani alipata kazi. Yuko kazini kwa kampuni ya maua ambapo anaishi." Alisema Rebecca.

Hata hivyo, waliskizana kuwa jumamosi atasafiri kwenda kupatana na