PATANISHO: Nilipata Rafiki Yangu Kitandani Mwetu Uchi Wa Mnyama

Bi Caroline, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe Fred, 28, kwani alimfumania na mpango wa kando na kisha akaamua kutoweka.

"Nilikuwa nimeelekea kazini wakti tulikuwa tunaishi Mombasa. Kufika kazini mwili haukuwa unahisi vyema kwa hivyo nikarudi nyumbani, kurudi nyumbani nikabisha mlango na bwanangu hakufungua kwa takriban dakika kadhaa.

Mwishowe alifungua lakini alikuwa amejifunga towel na nikamuuliza mbona hakuwa anafungua na nikaelekea hadi chumba cha kulala ili nilale. Kufika kitandani nikapata mwanadada mwingine akiwa uchi wa mnyama jinsi alivyo zaliwa." Alisema Caroline mwenye umri wa miaka 23, ambaye alidai jambo hilo lilimgadhabisha na hapo akafunga virago vyake na kuondoka.

"Tangia hapo hajawahi niongelesha na hadi wa sasa inakaa nikama mie ndiye niliyekuwa na makosa. Bado nampenda moyoni." Aliongeza akidai kisa hicho kilitokea mwezi wa Januari.

Alipopigiwa simu bwana Fred alikubali kuwa alifanya makosa.

"Kulikuwa na mrembo fulani rafikiye ambaye alikuwa ananisumbua, mke wangu akielekea kazini naye alikuwa anakuja kwangu kupiga ma story kabla nitoke nieleke kazini. Kutoka hapo akakuja siku moja akaniomba mia mbili, mwendo wa saa mbili akabisha mlango akaniambia hii maisha lazima tusaidiane kwani wewe sio mwanaume kamili?

Na hapo kwa yale majaribu nikamueleza kabla mke wangu arejee tutakuwa tumemaliza 'mission' na hapo bahati mbaya akatufumania." Alieleza bwana Fred.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be