PATANISHO: Nime move on na maisha na haturudiani!

Baba Akoth aliomba apatanishwe na mkewe bi Sharon aliyeondoka akisema walianza mizozo pindi tu alipo poteza kazi yake.

Nilisimamishwa kazi na baada ya hilo nikasema siwezi kaa Nairobi na nikaamua kupeleka familia yangu nyumbani. Mke wangu akasema kuwa hawezi enda nyumbani lakini ataishi Nairobi akitafuta kazi.

Alipopata kazi hatukuelewana na hapo tukatengana.

Wawili hao wamebarikiwa na watoto wawili katika ndoa ya miaka mitatu.

Sharon alipopigiwa simu alisema kuwa aliamua kuendelea na maisha yake na kamwe hayuko tayari kurudiana na bwana Martin.

Aii kurudiana naye haiwezekani kwa sababu nilijaribu hiyo ndoa na nikashindwa. Nilijaribu kwani hakuwa na kazi na nilipopata kazi hakuwa ananiamini na kuharibu mambo alikuwa ananichapa.

Siku moja nilirudi nyumbani nikapata amepeleka watoto nyumbani bila kuniarifu. Hapo nilienda kwa idara ya watoto na aliambiwa arudishe watoto na kitu alifanya ni eti alibeba mtoto aliyenioa naye na kuwacha mwenye tulipata naye.

Sahii nime move on na maisha na haiwezekani.

Bwana Martin alikiri makosa yake na kukubali kurudisha mtoto, hata hivyo Sharon alisema kuwa bado hayuko tayari kurudiana na bwanake.

"Kila akinichapa alikuwa anachukua hako katoto kadogo ananiwacha na yule mwingine kisha ananitafuta. Isitoshe sahii niko kwa ndoa na nashukuru mungu." Sharon alisema huku akiwashtua watangazi Gidi na Ghost.