PATANISHO: Nimebaki nikichekwa na Jamaa aliyeninyang'anya mke

patanisho
patanisho
Bwana Winston aliomba apatanishwe na mkewe bi Maureen, akidai walikosana na mkewe akamtenga.

"Kwanzia January niliwacha mke wangu Muhoroni nikienda Nairobi kwenda kutafuta kazi, juu mimi ndio nilimuweka Facebook na ilileta shida kwani kuna jamaa alinitumia ujumbe Whatsapp akisema anakatia mke wangu kwa inbox.

Kumuuliza mke wangu alisema kuwa nina wivu tu na mara kwa mara anapandisha mori na saa zingine hajibu simu zangu. Ilifika mahali nikamwambia awache zile tabia kwani ananiaibisha."

Winston alisema kuwa cha kuhuzunisha kuna mtu alimsaidia kubadilisha password na mara anapojaribu ujanja wa kuweza kusoma ujumbe wake anabadilisha password.

Isitoshe Winston alikuja kugundua kuwa mkewe amehama tayari na akabeba kila kitu kwa nyumba na kumuachia viti tu na cha kushangaza anasema kuwa jamaa aliyemnyang'anya mke amebakia kumcheka tu.

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka minane.

"Hayo ni maneno yake, sitaki kuskia maneno yake na nime move on na maisha yangu." Maureen alisema kabla ya kusitiza mawasiliano baina yetu.

Winston ambaye anakiri kuwa ndiye alimchanua mkewe kwa kumuingiza katika mitandao ya kijamii alimtakia mkewe kila la heri na baraka maishani mwake.