PATANISHO: Nimekubali nilipoteza mke wa maana - Evans

Evans alituma ujumbe akiomba apatanishwe na baba mkwe, babake aliyekuwa mkewe bi Patricia ambaye walikosana mwaka wa 2011.

"Tulikosana naye mwaka wa 2011 baada ya kukosana na mwanawe. Baba mkwe alikasirika baada ya kumpatia msichana wake kwa barabara baada yetu kukosana. Nilimwambia chukua mtoto wako kwani sioni kama tutaishi naye kwani tulikuwa tunavuragana kila wakati." Evans alisema.

Aliongeza,

Huyu baba mkwe kuna maneno alisema na naona maisha yangu hayaendi vyema kwani baadaye nilioa mke mwingine na tuliishi vyema na shida ni, wakati tulienda naye nyumbani na nikamuacha huko na nikarudi Nairobi lakini alipokuwa mgonjwa tulikuja tukawachana."

Evans anasema kuwa anataka wasameheane na baba mkwe ili warudiane na Patricia ambaye pamoja wamejaliwa watoto.

Juhudi zetu za kumpata baba mkwe hazikufua dafu na ilibidi tumpigie simu bi Patricia ambaye alisema kuwa waliwachana vibaya na tayari ameolewa.

Bi Patricia alimuarifu Evans,

"Wewe uombe daddy tu msamaha juu nishaolewa na nime settle, watoto ninao wawili wako sikatai kwani ni damu yako. Wewe ng'ang'ana tu uombe msamaha daddy juu ulimkosea hadi akalia."

Alisema kuwa Evans alimuacha barabarani na watoto akisema kuwa amechoka naye na kusahau kuwa alilazimika kuacha shule katika kidato cha pili na akamuachilia.

Patricia alisema kuwa amepata mume mwingine mzuri ambaye anampenda pamoja na watoto wake na anampenda.

Kwa upande wake, Evans aliomba kama Patricia anaweza zungumza na baba yake ili asamehewe.

"Sina kinyongo na wewe naomba upate mke mwingine, nakubali wewe ndiye baba watoto lakini siwezi rudiana nawe." Patricia alimuambia bwana Evans.

Evans alikubali kuwa yeye ndiye alisababisha yote na kuwa alikuwa na mke wa maana sana.