PATANISHO: Nimemalizana Nawe Ukitaka Oa Wanawake Tano!

John mwenye umri wa miaka 38, aliomba apatanishwe na mkewe Jane kwani walikosana mwezi uliopita, kisa na maana; John alikuwa na tabia za mipango ya kando.

"Kuna msichana alinipigia simu usiku tukiwa na bibi yangu na hapo tukakosana na mke wangu kwani yule alikuwa mpango wa kando. Ni shetani tu." Alieleza bwana John akidai kuwa walikuwa kwa uhusiano wa wiki moja pekee. John na mkewe wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne na wawili hao wamejaliwa watoto.

Kulingana na Jane, alikuwa anampata bwanake na mwanamke mwingine kwa nyumba huku wakati mwingine kupata mwingine akimtayarishia chai.

"Si unaona hiyo ni kazi? Unapata hata mwanamke yule yule amemtumia ujumbe akidai kuwa anahitaji ampe mapenzi." Alijieleza.

"Si ulikuwa ukitaka wenye wanakuonesha mapenzi na mimi hutaki mapenzi yangu? Nenda ukae nao sahii roho yangu imefika mwisho msamaha sitaki enough is enough. Nimemalizana nawewe sahizi ukitaka hata kuoa wanawake tano sina shida nawe, nilikusamehe nikachoka." Alimueleza mumewe akishikilia kuwa mapenzi yameisha kwa ajili ya madharau yake kwani hata akijilazimisha namna gani hawezi mpenda tena.

Aliongeza kuwa anahitaji miezi kama mitatu ili amsamehe na amrudie.